NEC yaongeza vituo

0
651

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeongeza vituo vya kuandikisha wapiga kura kutoka 36,549 vilivyotumika mwaka 2015 hadi 37,407  vilivyopo hivi sasa.

Idadi hiyo ya vituo imetolewa jijini Dar es salaam  na Mwenyekiti wa  NEC Jaji Semistocles Kaijage wakati wa mkutano wake na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini pamoja na wadau  wengine wa uchaguzi, katika kipindi hiki cha kuelekea zoezi la kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura.

Jaji Kaijage amesema kuwa tayari uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapiga kura limefanyika ili kuona kama kuna umuhimu wa kuongeza vituo vingine na kwa vilivyopo kuona kama bado vinakidhi matakwa ya kisheria.

Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura litaanza kwa majaribio katika kata mbili za Kihonda iliyopo kwenye Manispaa ya Morogoro na kata ya Kibuta iliyopo Kisarawe mkoani Pwani.