Ndyamukama Mkurugenzi Mkuu mpya TAA

0
339

Rais John Magufuli amemteua Mhandisi Julius Ndyamukama kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).

Mhandisi Ndyamukama anachukuwa nafasi ya Richard Mayongela ambaye uteuzi wake umetenguliwa na anatakiwa kuripoti wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambako atapangiwa kazi nyingine.

Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Ndyamukama alikuwa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Dar es Salaam na ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa ujenzi wa majengo namba 3 (Terminal 3) ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ambayo yapo katika hatua za mwisho kukamilika.

Uteuzi wa Mhandisi Ndyamukama unaanza leo Machi 26.