Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hivi karibuni kumekuwa na changamoto ya kuvunjika kwa ndoa nyingi jambo linalosababisha kuwepo na changamoto katika malezi ya watoto.
Akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii na Kilele cha Wiki ya Ustawi wa Jamii yaliyofanyika Mkoani Dar es Salaam, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka maafisa ustawi wa jamii kuimarisha familia ili watoto waweze kupata malezi bora kutoka kwa wazazi wote wawili.
Ameongeza kuwa watoto wanapolelewa na wazazi wawili ambao wametengana hujenga taifa ambalo halijatarajiwa.
Amewataka maafisa ustawi wa jamii kuwa mstari wa mbele kuongoza malezi ya familia hizo.