Ndege ya Kenya yashindwa kutua nchini humo

0
913

Ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) iliyokuwa ikitokea Lusaka, Zambia kwenda jijini Nairobi, Kenya imelazimika kutua kwa dharura mkoani Kilimanjaro, Tanzania baada ya kushindwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).

Ndege hiyo (KQ708) ilitoka Lusaka saa 9:35 alfajiri na ilitarajiwa kutua JKIA saa 1:35 asubuhi, lakini ilishindwa kutua kutokana na ukungu mzito uliokuwa umefunika uwanja.

Taarifa kutoka katika tovuti ya Flight Radar inaonesha kuwa ndege hiyo ilishindwa kutua baada ya kujaribu kufanya hivyo mara mbili, ndipo ikaelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ambapo ilitua saa 8:25 asubuhi.