Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), leo imeshindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera kutokana na hali mbaya ya hewa.
Habari zaidi zinaeleza kuwa, badala yake rubani wa ndege hiyo alilazimika kurejea Mwanza na kutua salama.
Taarifa zinaeleza kuwa ndege hiyo ya Air Tanzania ilishindwa kutua katika uwanja huo wa ndege wa Bukoba kutokana na kuwepo kwa ukungu, mvua, radi na giza na hivyo uwanja ukawa hauonekani.
Baada ya tukio hilo, katika ukurasa wake wa Instagram Mbunge wa Viti Maalum Neema Lugangira ameandika
“Still shaken [bado natikiswa] lakini Mungu ni mwema. Nimepanda ndege asubuhi ya leo kwenda Bukoba. Safari ilikuwa na changamoto, tumefika lakini ndege ikashindwa kutua. Nampongeza rubani kwa uamuzi sahihi wa kurudi Mwanza na sasa narudi Dar. Serikali ibebe kwa uzito suala la airport mpya Bukoba”.