Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kufuatia maafa yaliyotokea Kijiji cha Katesh Wilayani Hanang Mkoani Manyara leo na kusababisha vifo vya zaidi ya Watu 20 hadi sasa ambapo ametoa maelekezo kwamba nguvu zote za Serikali zielekezwe kwenye uokozi na kuzuia maafa zaidi kutokea.
Akiongea kutokea Dubai Rais Samia amesema “Kwa masikitiko makubwa tumepokea taarifa za kutokea kwa mvua kubwa Mkoa wa Manyara na kuleta madhara makubwa katika Kijiji cha Katesh, sisi tuliopo huku (Dubai) ambao tunashikiri mkutano wa mazingira tumesikitishwa sana na tukio hili lakini mipango ya Mungu ndivyo inavyokwenda tunatoa pole kwa Wahanga wa tukio hili”.