Natamani kuiona hapa studio ya kisasa mwakani

0
124

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema anatamani kuona Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) linakua na studio kubwa na za kisasa katika viwanja vya Sabasaba yanapofanyika maonesho ya kimataifa ya biashara kila mwaka.
  
 
Amesema uwepo wa studio za TBC katika viwanja vya Sabasaba utawahakikisha watanzania uwepo wa TBC katika viwanja hivyo kila yanapofanyika maonesho hayo.
 

 
Waziri Nape ametoa kauli hiyo mkoani Dar e Salaam alipotembelea banda la TBC lililopo katika viwanja vya Sabasaba yanapofanyika maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja hivyo
  
 
Aidha, amesema anafurahishwa kuona namna taasisi zilizo chini ya wizara Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari zinavyosaidia kuifanya Tanzania kuwa sehemu nzuri ya kuwekeza akitolea mfano wa namna Shirika la Utangazaji Tanzania linavyotangaza habari mbalimbali zinasaidia kuyafahamu maeneo ya uwekezaji.