NARCO yavunja mkataba Karagwe

0
131

Bodi ya kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) imevunja mkataba na mwekezaji Agro Business wa kitalu namba moja katika ranchi ya Kitengule iliyopo wilayani Karagwe mkoani Kagera.

Hatua hiyo inafuatia eneo la kitalu hicho kutumika kusafirisha magendo ikiwemo ng’ombe na pembe za ndovu kwenda nchi jirani.

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Karagwe imemweleza mwenyekiti wa bodi ya NARCO Mhandisi Cyprian Luhemeja kuwa, ilifanya uchunguzi na kubaini mwekezaji huyo hakuwa na mifugo katika ranchi hiyo na kuwa amewakodishia wafugaji wengine kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 200 kwa mwaka.

Bodi ya kampuni ya Ranchi za Taifa ipo mkoani Kagera, kwa lengo la kukagua na kutembea ranchi mbalimbali zinazopatikana mkoani humo.