Nape atoa siku 14 kwa maofisa habari

0
239

Waziri wa habari mawasiliano na teknolojia ya habari, Nape Nnauye ametoa siku 14 kwa tovuti na taasisi zote za serikali,kuwa na taarifa zinazoendana na wakati ili wananchi waweze kufahamu kazi kubwa inayofanywa na serikali katika kuwaletea maendeleo watanzania.

Waziri Nape ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa kikao cha 17 cha maafisa habari, mawasiliano na uhusiano wa serikali kilichofanyika jijini Tanga.

Amesema kazi kubwa ya maafisa habari ni kusema na kuonyesha kazi za serikali na si vinginevyo, hivyo hata wavumilia maafisa habari watakaoenda kinyume na agizo hilo.

Amesema katika kufuatilia jambo hili idara ya habari Maelezo inapaswa kutengeneza mfumo maalum wa ufuatiliaji na upimaji wa majukumu ili kuleta chachu ya mabadiliko katika kutekeleza wajibu wa utumishi kwenye sekta ya habari mawasiliano na teknolojia ya habari.