Namna rahisi ya kulinda figo yako

0
521

Daktari bingwa wa figo aeleza kuwa ulinzi wa figo unaweza kufanywa kwa kuzingatia yale ambayo mtu hufanya ili kulinda moyo wake.

Dkt. Muhdini Mahmoud ameeleza kuwa chochote ambacho ni hatarishi kwa moyo wako ni hatarishi kwa figo pia na kinyume chake kutokana na mahusiano ya ukaribu kati ya viungo hivyo viwili. Hii ndio sababu magonjwa ya moyo hupelekea magonjwa sugu ya figo.

Aidha, ameilezea TBC kuwa figo inahitaji 20% hadi 25% ya kiwango cha damu inayosukumwa na moyo kwa dakika.

Baadhi ya magonjwa ya maambukizi ikiwemo; kifua kikuu, homa ya ini, na malaria huweza kupelekea athari kwenye figo.

Inashauriwa kunywa maji angalau lita moja na nusu kwa siku ili kuisaidia figo yako kufanya kazi vyema na kutoa sumu mwilini.