Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imemzawadia Rais Mstaafu wa Pili, Ali Hassan Mwinyi gari jipya aina ya Mercedes Benz ili kumsaidia kufanya shughuli zake, kwani gari la awali lilikuwa juu saa hivyo kumpa changamoto kupanda.
“Nimemuandalia zawadi Mzee Mwinyi, kwa kutimiza umri wa miaka 96 leo, nimekuwa nikiona usumbufu anaoupata akiwa anapanda na kushuka kwenye gari lake, kwa niaba ya Serikali, Mzee wetu leo tutampatia Benz la chini ambalo litampa raha kwenye Safari zake,” amesema Rais Samia Suluhu Hassan.