Mwili wa Mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Festo Sikagonamo aliyefariki dunia usiku wa kumkia hii leo katika hospitali ya rufaa Kanda ya Mbeya, unaagwa mchana huu nyumbani kwake eneo la Soweto mkoani Mbeya.
Baada ya shughuli hiyo ya kuaaga, mwili wa Festo utasafirishwa kwenda kijiji cha Kifunda wilayani Rungwe kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika hapo kesho.
Festo alikuwa ni Mwandishi wa habari wa TBC kituo cha Mbeya.