Mwili wa Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Bernard Membe tayari umewasili kijijini kwao Rondo mkoani Lindi, ukitokea Dar es Salaam.
Mwili wa Membe umesafirishwa leo kwa helkopta ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Mazishi ya Membe yatafanyika hapo kesho katika kijiji hicho cha Rondo na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki pamoja na viongozi mbalimbali.
Bernard Membe alifariki Dunia Mei 12, 2023 katika hospitali ya Kairuki mkoani Dar es Salaam.