Mwili wa Marin Hassan Marin wazikwa visiwani Zanzibar

0
355

Mwili wa aliyekuwa Mtangazaji Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Marin Hassan Marin umezikwa leo asubuhi huko Mwanakwerekwe visiwani Zanzibar.

Marin alifariki dunia alfajiri Aprili Mosi 2020 katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, jijini Dar es Salaam baada ya kuugua ghafla akiwa nyumbani kwake.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria mazishi hao wamemuelezea Marin kama shujaa aliyebobea katika tasnia ya habari.

Marehemu alizaliwa Julai 15, 1972. Alihitimu elimu ya stashahada ya uandishi wa habari mwaka 2004.

Marehemu aliajiriwa na iliyokuwa Taasisi ya Utangazaji Tanzania kuanzia Mei 01, 2005 kama mwandishi wa habari daraja la II. Marehemu alipanda madaraja mbalimbali hadi kufikia katika cheo cha Mwandishi wa Habari Mwandamizi cheo alichokuwa nacho mpaka umauti ulipomfika.