Mwili wa Maalim Seif waagwa Dar, wapelekwa Unguja

0
258

Mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, umeagwa mapema leo asubuhi katika Msikiti wa Maamur, Upanga, jijini Dar es Salaam kabla ya kupelekwa Zanzibar kwa ajili ya mazishi.

Dua maalum ya kumuombea Maalim Seif imeongozwa na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi, ambapo amesema kuwa msiba huu umeathiri watu wengi kwa sababu Maalim Seif alikuwepo kwa ajili ya Watanzania wote.

Akizungumza wakati wa dua hiyo Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, amesema kuwa watu wanajua juhudi ambazo Maalim Seif alizifanya, na si kwa Wazanzibar pekee bali kwa Watanzania wote na kwamba ataendelea kukumbukwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Zanzibar.

Maalim Seif atazikwa leo Februari 18, 2021, huko Mtambwe, Pemba visiwani Zanzibar.