Mwili wa Balozi Kijazi kuagwa leo Dar es Salaam

0
226

Mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi unaagwa leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kisha utasafirishwa kwenda Korogwe, Tanga kwa ajili ya maziko.

Shughuli za kuaga mwili huo zinaongozwa na Rais Dkt. John Magufuli na pia zitahudhuriwa na viongozi mbalimbali.

Balozi Kijazi alifariki dunia Februari 17, 2021 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu.

Usikose kufutilia matangazo mbashara kupitia TBC1, TBC Taifa na kurasa zetu za Facebook na YouTube kwa jina la TBCOnline.