Mwili wa Amry wa TBC waagwa

0
226

Mwili wa dereva wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Rajab Amry aliyefariki dunia usiku wa kuamkia terehe 30 mwezi huu akiwa safarini kikazi mkoani Arusha umeagwa hii leo nyumbani kwake Tandika mkoani Dar es Salaam.
 
Mwili wa Amry umeagwa na ndugu, jamaa, marafiki, majirani pamoja na wafanyakazi waliokuwa wakifanya naye kazi.

Mara baada ya kuagwa mkoani Dar es Salaam, mwili wa dereva Amry unasafirishwa kuelekea mkoani Mwanza kwa ajili ya mazishi.
 
Rajab Amry aliajiriwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) mwezi Mei mwaka 2005 akiwa dereva Mwandamizi na kupanda madaraja hadi kufikia Dereva Mkuu.
 
TBC itamkumbuka marehemu Amry kwa wema wake, uchapakazi, kujitolea na ushirikiano kwa miaka yote 17 aliyolitumikia shirika lhilo.