Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unatarajiwa kufanyika keshokutwa Ijumaa jijini Dodoma.
Miongoni mwa kazi kubwa za mkutano huo ni kumchagua Mwenyekiti wa CCM Taifa.
CCM inamchagua Mwenyekiti wake mpya kufuatia kifo cha Dkt. John Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, kilichotokea Machi 17 mwaka huu.
Ìngawa CCM haijaweka wazi atakayechaguliwa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, – Humphrey Polepole aliwahi kuwaeleza Waandishi wa habari mara baada ya kikao maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kilichofanyika jijini Dodoma Machi 30 mwaka huu kuwa, atakuwa Rais wa sasa Samia Suluhu Hassan ambaye atakwenda kupigiwa kura.