Mwenge wawasili Morogoro: Adha ya mafuriko yatatuliwa

0
203

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa Lt. Josephine Mwabashi amezindua mfereji wa maji uliopo manispaa ya Morogoro utakaosaidia kuondoa adha ya mafuriko kwa wafanyabiashara na wananchi wa manispaa hiyo.

Mbali na kuzindua mfereji huo, Mwambasha amewasihi viongozi wanaohusika na mfereji kuzingatia usafi ili kutosababisha mfereji kuziba na kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Mbio za Mwenge zilizinduliwa rasmi Mei 17 , Zanzibar na zinatarajiwa kumalizika Oktoba 14, 2021 Geita.