Mwenge waridhishwa na ujenzi wa barabara

0
323

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka huu Abdallah Shaib Kaim ameeleza kuridhishwa na ujenzi wa barabara kutoka barabara Kuu kwenda hospitali ya Kanda ya Kusini eneo la Mitengo kwa kiwango cha lami.

Amesema barabara hiyo inayojengwa na Wakala na Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wilaya ya Mtwara, ubora wake unalingana na thamani ya fedha.

Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka huu amesema hayo wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Mitengo – hospitali , yenye urefu wa kilomita moja ambayo
hadi kukamilika kwake ujenzi wake utakuwa umegharimu shilingi milioni 500.

Aidha, amewaomba Wananchi kuitunza barabara hiyo pindi itakapokamilika ambayo kwa sasa ujenzi wake umefikia asilimia 80.