Mwenge wabisha hodi Mkuranga

0
182

Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake wilayani Mkuranga mkoani Pwani, ambapo pamoja na mambo mengine utapitia miradi 12 yenye thamani ya shilingi Bilioni 500.9.

Akipokea Mwenge huo mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Khadija Nasri Ali amesema fedha za miradi hiyo ni matokeo ya kazi kubwa inayofanywa Serikali ya kupeleka maendeleo kwa Wananchi wa Mkuranga.

Amesema miongoni mwa miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru wilayani Mkuranga ni kituo cha afya Nyamato, shule ya sekondari Kilimahewa na mradi wa uhifadhi wa mazingira na chanzo cha maji katika kijiji cha Njopeka.