Mwenge waanza mbio zake Tandahimba

0
198

Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa kwa uongozi wa wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, baada ya kumaliza mbio zake wilayani Mtwara.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Hanaf Msabaha akikabidhi Mwenge huo kwa mkuu wa wilaya ya Tandahimba Kanali Patrick Sawala amesema, ukiwa wilayani Mtwara Mwenge wa Uhuru uliona, kukagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi 16 ya maendeleo.

Aidha amesema Mwenge wa Uhuru umeridhia miradi yote iliyotembelea katika wilaya ya Mtwara na hakuna mradi uliokataliwa.