Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro ambapo utakagua, kutembelea na kuzindua miradi saba yenye thamani ya shilingi bilioni mbili.
Akizingumza mara baada ya kukabidhiwa Mwenge huo, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Raymond Mangwala ametaja miradi hiyo kuwa ni ya afya, elimu, barabara na maji. Amesema Mwenge pia utatembelea vikundi vya wajasiriamali.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu.’