Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake mkoani Pwani ambapo ukiwa mkoani humo utapitia miradi 126 yenye thamani ya shilingi Trilioni 8.53.
Mkuu wa Mkoa Pwani, Abubakari Kunenge amesema ukiwa katika mkoa huo, Mwenge wa Uhuru utapitia miradi 126 iliyoko katika halmashauri tisa za mkoa huo ambapo miradi 18 itawekewa mawe ya msingi, 22 itakaguliwa na miradi 16 itazinduliwa.
Baada ya Mwenge wa Uhuru kupokelewa mkoani Pwani umekimbizwa katika halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo ambapo mkuu wa wilaya hiyo Halima Okashi amesema utapitia miradi 29 yenye thamani ya shilingi Bilioni 15.2.