Mwenendo wa ATCL waimarika

0
181

Mwenendo wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kwa mwaka wa fedha 2021/2022 umeimarika ikilinganishwa na mwaka wa fedha uliopita wa 2020/2021.

Taarifa hiyo imetolewa jijini Dodoma na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Dkt. Charles Kichere wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.

Amesema kampuni hiyo imeongeza mapato kwa asilimia 11 na kupunguza matumizi kwa asilimia tatu, huku ikipunguza hasara kutoka shilingi bilioni 60.25 katika mwaka wa fedha wa 2019/2020 hadi kufikia shilingi bilioni 36.18 mwaka wa fedha wa 2020/2021.

Aidha Dkt. Kichere amesema kampuni ya Mkulazi imekuwa ikipata hasara kwa miaka mitano mfululizo tangu mwaka wa fedha wa 2016/2017.