Mwanza waokoa bilioni moja ujenzi wa madarasa

0
182

Ujenzi wa vyumba 64 vya madarasa ya ghorofa katika halmashauri ya Jiji la mwanza umewezesha halmashauri hiyo kuokoa zaidi ya shilingi billioni moja ambazo zingetumika kununua ardhi pamoja na kulipa fidia.

Uamuzi wa halmashauri ya Jiji la Mwanza wa kujenga madarasa ya ghorofa ili kukabiliana na tatizo la ardhi umepongezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini (ALAT) Murshid Ngeze ambaye amezitaka halmashauri nchini kuiga mfano huo ili kuokoa fedha za umma

Ujenzi huo wa vyumba 103 vya madarasa umeboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia katika wilaya ya nyamagana Jijini Mwanza

Vyumba hivyo vikiwemo 64 vinavyojengwa kwa mfumo wa ghorofa vimegharimu zaidi ya shilingi billioni tatu zikiwemo billion 1.9 za Uviko-19 pamoja na billioni 1.2 za mapato ya ndani ya halmashauri ya Jiji la mwanza