Mwanza tayari kupunguza ajali za barabarani

0
124

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Adam Malima amesema mkoa huo upo tayari kuhakikisha ajali zinazosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali zinamalizwa na mkoa huo kuwa salama.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Kitaifa mkoani Mwanza, Malima amesema, watu 96 wamefariki dunia katika kipindi cha mwaka 2022 mkoani humo kutokana ajali 81 kubwa za magari pamoja na ajali 30 za pikipiki huku ajali hizo zikiacha majeruhi 122.

Aidha Malima ametoa rai kwa watumiaji wa vyombo vya moto na barabara mkoani Mwanza, kufuata sheria za barabarani wakati wote.

Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanafanyika mkoani Mwanza kuanzia Marchi 13 hadi 17, 2023 yakiwa na kauli mbiu inayosema kuwa “Tanzania bila ajali inawezekana, Timiza Wajibu wako”.