Mwanamuziki mkongwe kutoka Afrika Kusini, Bulelwa Mkutukana maarufu Zahara, mshindi wa tuzo mbalimbali amefariki dunia Jumatatu usiku alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali jijini Johannesburg.
Mwanamuziki huyo aliyetamba kwa vibao mbalimbali ikiwa ni pamoja na ‘Loliwe’ alikuwa akipambania uhai wake kutokana na ugonjwa wa ini wiki mbili zilizopita.
Zahara alikuwa mwanamuziki mahiri ambaye alitumia gitaa kukonga nyoyo za wapenda burudani, hivyo kuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya burudani barani Afrika.
Hivi karibuni Zahara alitoa albamu tano ambazo zilikuwa na mapokeo makubwa kwa mashabiki wake akitamba na mziki wa Nqaba Yam (2021).
Zahara ameshinda jumla ya tuzo 17 za muziki za Afrika Kusini pamoja, tuzo 3 za Metro FM na tuzo 1 ya tuzo za burudani Nigeria.