Mwamposa na wenzake wahojiwa na polisi

0
450

Jeshi la Polisi Tanzania, limemuhoji Boniface Mwamposa na Waandaaji wa kongamano lililosababisha vifo vya watu 20 na wengine 16 kujeruhiwa mjini Moshi.

Vifo hivyo vilitokea wakati waumini wakigombania kukanyaga mafuta ya upako wakati wa mkutano wake uliofanyika kwenye Uwanja wa Majengo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi, Mwamposa na wenzake waliohusika kuandaa kongamano hilo wametoa maelezo yao kuhusu kile kilichotokea na kusababisha vifo vya watu 20

Pia, taarifa hiyo imeeleza kuwa serikali itachukua hatua stahiki endapo itabaini kuna kosa la jinai lililosababisha vifo hivyo na majeruhi na kutumia mapungufu hayo kujiimarisha kuzuia hali hiyo kutojirudia.

“Mapungufu watakayoyabaini katika uchunguzi huo yatasaidia kuweka mikakati thabiti ili kuepusha madhara kama hayo kutokea katika mikusanyiko mbalimbali,” -amesema Mtendaji Mkuu wa Jeshi la Polisi, Davide Misime- SACP.