Mwalimu alikua muumini wa usawa wa kijinsia

0
182

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema katika maisha yake Mwalimu Nyerere aliongozwa na falsa ambazo ndio ziliendesha Siasa na kuendesha nchi.

Profesa Mkenda amesema, Mwalimu pia alikua na muumini wa usawa wa kijinsia kwa vitendo na aliishi imani hiyo.

Akizungumza katika kongamano la miaka 100 ya kumbukizi ya miaka 100 ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Mwalimu Nyerere Profesa Mkenda amesema falasa ya usawa wa kijinsia ya Mwalimu leo imeishi kwa vitendo

Waziri Mkenda ameongeza kuwa Mwalimu akiwa chuoni Makelele Uganda aliandika andiko ambalo linahusiana na usawa wa kijinsia na hata baada ya kuwa madarakani aliendelea kusimamia jambo hilo kwa vitendo