Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), mvua itaendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali nchini kwa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku leo, Februari 13.
Hali ya mawingu, mvua, ngurumo na vipindi vya jua inatarajiwa katika mikoa mbalimbali ya Mbeya, Rukwa, Iringa, Songwe,Njombe, kusini mwa Mkoa wa Morogoro, Ruvuma, Kigoma, Katavi, Tabora, Dodoma, Singida.
Maeneo ya Kagera,Geita, Shinyanga, Mwanza, Mara, Simiyu, Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Lindi, Unguja, Pemba, Pwani pamoja na Kisiwa cha Mafia yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua, ngurumo na vipindi vya jua.
Kwa upande wa mikoa ya Kilimanjaro, Manyara na Arusha zinatarajiwa itakuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua pamoja na ngurumo.
Katika utabiri huo, TMA imeitaja maeneo ya Tanga na Zanzibar kwamba yatakuwa na joto zaidi kwa nyuzi joto 32°C huku mkoa wa Njombe ukiwa hali joto ya chini 13°C hadi 20°C.
TMA imetoa angalizo kwa wananchi wa Songwe, Ruvuma, Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora na kusini mwa Morogoro juu ya mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha.