Mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Mussa Idd Mussa amefariki dunia alfajiri ya leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili mkoani Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu.
Mwili wa Mussa ambaye alikuwa Mtumishi wa TBC, utaagwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili saa saba mchana hii leo.
Baadaye leo, utasafirishwa kwenda nyumbani kwao Pangani mkoani Tanga kwa ajili ya mazishi.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi Amina.