Muro: Vijana tufuatilie ajenda zenye maslahi

0
444

Mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Jerry Muro, amewataka vijana katika nchi za Afrika kuzungumzia ajenda zitakazokuwa na maslahi mapana katika nchi zao ili kuleta tija katika ukuaji wa kiuchumi.

Muro akizungumza hayo jijini Arusha,wakati wa akifunga mkutano kivuli wa vijana wa umoja wa mataifa uliofanyika kwa siku mbili,ambao uliwakutanisha vijana miambili kutoka katika mataifa mbalimbali Duniani, Muro amesema vijana wana fursa nyingi ambazo zikitumika vema nchi za Afrika zitanufaika.