Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia mtu mmoja na kuwasaka wengine wawili kwa tuhuma za kuwaua kikatili watu wawili ambao ni mume na mke, na kisha kutelekeza miili yao katika maeneo tofauti.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya, -Ulrich Matei amesema mauaji hayo yametokea katika kata ya Iyela na kuwataja waliouawa kuwa ni Samson Ndavi aliyekuwa akifanya kazi ya ulinzi pamoja na mke wake Christina Mwakilembe.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, – Albert Chalamila amefika katika eneo la tukio kwa ajili ya kutoa pole kwa familia ya marehemu hao na kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoa humo kufanya uchunguzi zaidi wa tukio hilo ili kuwabaini na kuwakamata wahusika wote.