MULAMULA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UAE

0
230

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi LIberata Mulamula amesaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) nchini, kufuatia kifo cha Rais wa Umoja huo Sheikh Khalifa Bin Zayed Al-Nahyan kilichotokea tarehe 13 mwezi huu.

Baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa UAE uliopo mkoani Dar es Salaam, Balozi Mulamula ametoa salamu za pole kwa Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu na kuwasihi wananchi wa nchi za umoja huo kuendelea kuwa watulivu wakati wa kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na kiongozi wao.