Muitikio wa kuchoma Chanjo ya UVIKO – 19 washika kasi

Chanjo Uviko - 19

0
201

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ameungana na Watanzania kuitikia wito wa kuchanja chanjo ya kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO 19.

Mahundi amepata chanjo hiyo Kituo cha Oysterbay katika viwanja vya Farasi mkoani Dar es Salaam mara baada ya mbio za marathon zilizoongozwa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ambapo pia imewekwa kambi ya kutoa chanjo.

Katika zoezi hilo waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuuweka mwili katika hali ya utimamu.

Zoezi la utoaji wa chanjo ya UVIKO19 limezinduliwa Ikulu jijini Dar es Salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Julai 28 mwaka huu