Mufti wa Tanzania atoa tamko vifo vya wanafunzi 10 Kagera

0
544

Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuberi, amewataka wamiliki wote wa shule za kiislamu nchini kuimarisha ulinzi pamoja na kuboresha miundo mbinu ya umeme ili kudhibiti matukio ya moto ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara katika baadhi ya shule.

Mufti ametoa rai hiyo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari makao makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) jijini Dar es Salaam kufuatia tukio la moto lililotokea siku chache zilizopita katika Shule ya Msingi Byamungu Islamic iliyopo Kyerwa, Kagera na kusababisha vifo vya wanafunzi kumi na wengine kujeruhiwa.

Aidha, Mufti Zuberi ametoa pole kwa waislamu na wazazi wote waliofikwa na msiba huo na kuwataka kuwa na subira kipindi hiki kigumu wakati vyombo vya usalama vikiendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.