Mufti wa Tanzania amteua katibu Mkuu wa Bakwata

0
548

Mufti wa Tanzania Shekhe Abubakar Zubery amemteua na kumthibitisha rasmi Ustadh Nuhu Jabir Mruma kuwa katibu mkuu wa BAKWATA

Mruma ambaye amekaimu nafasi hiyo tangu mwezi wa nne mwaka 2018 amethibitishwa leo tarehe 5 Juni 2019 na Mufti wa Tanzania kushika nafasi hiyo