Mtwara watakiwa kusalia kwenye vituo

0
461

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, – Gelasius Byakanwa amewatoa hofu wakazi wa mkoa huo na kuwataka kuendelea kusalia kwenye vituo ambavyo serikali ya mkoa huo imewaelekeza wakae  kwa muda kwa hofu ya Kimbunga Kenneth, vituo vinavyodaiwa kuwa ni salama.

Akizungumza na wakazi waliokusanyika katika eneo la uwanja wa Ndege wa Mtwara, – Byakanwa amesema kuwa hadi sasa hakuna madhara yoyote yaliyotokea na kuwataka wakazi wa mkoa huo kupuuza na kutoamini habari zinazosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba hali ya Mtwara si shwari.