Mtoto auawa kikatili

0
207

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mkazi mmoja wa kijiji cha Mese wilayani Siha kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mtoto wa kaka yake kwa kumkata na kitu chenye ncha kali.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema kabla ya tukio hilo mtuhumiwa alichukua panga la kukatia majani ya ng’ombe na kuelekea kwenye banda la ng’ombe na kumkata ndama shingoni na kufa papo hapo.

Kamanda Maigwa amesema baada ya kufanya tukio hilo ndipo mtuhumiwa alienda alipo mkewe ambapo alikuwa na mtoto huyo wakinywa chai na kutekeleza mauaji ya mtoto huyo kwa kumkata shingoni kwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili.

Maigwa amemtaja mtoto aliyeuwawa kuwa ni Johnson Roland mwenye umri wa miaka sita huku akibainisha kuwa mtuhumiwa anahisiwa kuwa na ugonjwa wa akili.

Hata hivyo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo.