Mkutano wa 14 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza jijini Dodoma.
Mkutano huo umeanza kwa kuapishwa kwa Mbunge mteule wa jimbo la Temeke mkoani Dar es salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdallah Mtolea.
Mtolea alitangazwa kupita bila kupingwa mwezi Disemba mwaka 2018 baada ya Novemba 15 mwaka huohuo wa 2018 kutangaza Bungeni jijini Dodoma kukihama Chama Cha Wananchi (CUF) na kuhamia CCM.
Baada ya kiapo hicho Spika wa Bunge, -Job Ndugai alitoa taarifa kwa Bunge kuhusu kusainiwa kwa Muswada wa Sheria Ndogo za Fedha wa mwaka 2018, na hivyo kuwa sheria kamili.