Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu ameongoza katika kura za maoni za kuwania ubunge jimbo la Singida Mashariki baada ya kuwashinda wagombea 13 waliokuwa wanawania nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Msimamizi wa uchaguzi huo, Salum Reja ametangaza majina ya wagombea walioshika nafasi za juu katika matokeo hayo ya kura ya maoni katika Chama Cha Mapinduzi.
Uchaguzi mdogo katika jimbo la Singida Mashariki unatarajiwa kufanyika Julai 31 mwaka huu.