Mtatiro aanza kazi Shinyanga

0
765

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Julius Mtatiro ameripoti kwenye kituo chake kipya cha kazi wilayani Shinyanga,
ili kuanza kutekeleza majukumu yake.

Katika kikao kifupi cha makabidhiano ya ofisi kilichohudhuriwa na Kamati ya Usalama ya wilaya ya Shinyanga, Mtatiro amekabidhiwa nyaraka mbalimbali na kueleza kuridhishwa na kasi ya maendeleo wilayani humo na kuahidi kushirikiana na viongozi wengine, wadau na wananchi wote ili kuleta maendeleo zaidi katika wilaya hiyo.