Mtandao wa viongozi Wanawake Afrika tawi la Tanzania wazinduliwa

0
174

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa, Tanzania imevuka uwiano uliowekwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa Wanawake kushiriki katika nafasi za maamuzi na uongozi.

Makamu wa Rais amesema hayo jijini Dodoma katika uzinduzi wa mtandao wa viongozi wanawake Afrika tawi la Tanzania.

Uzinduzi huo unaifanya Tanzania kuwa nchi ya 14 kuingia katika mtandao huo wa viongozi Wanawake Afrika, tangu ulipoanzishwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2017.