Mshirikiane kutunza Mazingira

0
146

Mwenyekiti wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) Askofu Charles Kasonde, amewataka viongozi wa kisiasa kutoka nchi wanachama wa shirikisho hilo kushirikiana katika mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira Barani Afrika.

Askofu Kasonde ameyasema hayo kwenye mkutano wa 20 wa AMECEA unaoendelea mkoani Dar es Salaam, ambapo Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi.

Amesema viongozi wa Mataifa ya Afrika wakishirikana na Shirikisho hilo watafanikiwa kwa kiasi kikubwa kulinda na kutunza mazingira ndani ya mataifa hayo.

Askofu Kasonde ameongeza kuwa kila mwanandamu ana wajibu wa kutunza mazingira kama ilivyokuwa tangu kuumbwa kwa Dunia na hata vitabu vya dini vinasisitiza utunzaji wa mazingira.