MSD Kujenga Ghala Arusha

0
247

Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongella ameuhakikishia uongozi wa Bohari ya Dawa (MSD) kuwa ataukabidhi eneo la ujenzi wa ghala la kuhifadhi dawa kwa mkoa huo kabla ya Januari 2024 ili kurahisisha usambazaji wa dawa mkoani humo.

Mongella amesema hayo katika kikao kazi cha Bohari ya Dawa (MSD) na wateja wake kanda ya Kilimanjaro kilichofanyika mkoani Arusha na kuipongeza kwa kusambaza dawa na vifaa tiba nchi nzima pamoja na uwepo wa changamoto za miundombinu kwa baadhi ya maeneo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai amesema mamlaka hiyo imedhamiria kupunguza kwa kiasi kikubwa uagizaji wa bidhaa za afya kutoka nje ikiwemo kuongeza uzalishaji nchini.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Damas Kayera amesema mbali na changamoto zilizopo, MSD inaendelea kupiga hatua kwa kuhakikisha dawa zinafika kwa wakati ambapo sasa usambazaji unafanyika kila baada ya miezi miwili.