Msando alipa deni la matibabu ya Mama aliyefariki Muhimbili

0
217

Wakili wa kujitegemea nchini Albert Msando amekabidhi Shilingi Milioni Tano, alizozikusanya kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, kwa ajili ya kulipia deni la matibabu ya mama aliyefariki Dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo jijini Dar es salaam na familia yake kushindwa kumudu deni la gharama za matibabu.

Siku chache zilizopita, mtoto wa marehemu alimlilia Rais John Magufuli aliyekwenda kuwatembelea majeruhi wa ajali ya moto ya Morogoro na kumuomba hela ya kulipia deni la matibabu la zaidi ya Shilingi Milioni Tano, ili aweze kutoa maiti ya mama yake.

Msando amekabidhi fedha hizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, – Profesa Lawrance Museru.