Msamaha kwa wanaomiliki silaha haramu

0
137

Jeshi la Polisi nchini limesema kutakuwa na kampeni maalum inayojulikana kama msamaha wa Afrika itakayohusisha usalimishaji wa silaha haramu kwa hiari zinazomilikiwa na baadhi ya watu kinyume cha sheria, ama kwa kutokujua taratibu za kisheria za umiliki wa silaha hizo.

Akitoa taarifa hiyo leo msemaji wa Jeshi la Polisi nchini kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP-David Misime amesema uzinduzi wa kampeni hiyo utafanyika tarehe Septemba 05, 2022 katika viwanja vya mashujaa mkoa Dodoma.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na Jeshi hilo ili kufanikisha usalimishaji wa silaha hizo kwani atayesalimisha silaha ndani ya muda uliotengwa hatochukuliwa hatua za kisheria