Msalaba Mwekundu waadhimisha miaka 62

0
239

Sherehe za maadhimisho ya miaka 62 ya Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) kitaifa zinafanyika jijini Dodoma ambapo wanachama wa chama hicho kutoka mikoa mbalimbali nchini wamehudhuria katika maadhimisho hayo.

Chama hicho huisaidia serikali katika utoaji wa huduma za misaada ya kibinadamu kwenye maeneo ambayo hutokea majanga yanayoathiri maisha ya watu.

Maadhimisho haya yamebeba kaulimbiu isemayo “Natoa kwa furaha na furaha ninayotoa ni zawadi.”

Jiulize: Nawe unatoa na kujitoa kwa wengine kwa furaha? Au unatoa ukiwa umenuna?