Msafara wa Makamu wa Pili wa Rais wapata ajali

0
115

Mtu mmoja amefariki dunia na wawili kujeruhiwa baada ya gari lililobeba waandishi wa habari katika msafara wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla kupata ajali mapema leo.

Ajali hiyo imetokea eneo la Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja.

Aliyefariki katika ajali hiyo ni mhudumu wa Habari Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Hamis Mchenga.

Aidha, waliojeruhiwa ni mpigapicha Kassim na mwandishi wa habari Hassan Issa, wote kutoka ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.